Miss Shinyanga Aelezea Sababu Za Kumchukia Mc Pilipili
Msanii wa kike wa nyimbo za injili Nicole Franklin Sarakikya ambae pia alishawahi kushiriki mashindano na kushinda Miss Shinyanga amefunguka na kuelezea kuhusu mahusiano yake na kukubali juu ya baba wa mtoto wake,Nicole ambae ana mtoto mmjoa wa kiume aliyezaa na mbunge wa singida Ery Kingu, anakubali kuwa ndie baba wa mtoto na anasema kuwa baba huyo anamuhudumia vizuri mtoto wake lakini kwa sasa hawana mahusiano ya kimapenzi ila wanawasiliana kama wazazi. ” ni kweli Erry Kingu ni baba wa mtoto wangu , Gideon” alisema Nicole
Kuhusu yeye kujua kuwa baba wa mtoto ni mume wa mtu nicole anasema kuwa ana muheshimu sana mke wa mzazi mwenzie “namuheshimu sana yule mama , she is so humble na sijui kama anajua”
Katika mahojiano yake na Spin Tv, anasema sababu za yeye kuachana na baba mzazi wa mtoto wake al “hata sijui sababu, mara nyingine hutokea, watu wanaachana bila kuwa na sababu labda yeye anajua, na wala sijutii kuwa nae kwa sababu amenipa baraka, mtoto ni baraka”
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Nicole alishawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchekeshaji na mshereheshaji maarufu Mc Pilipili , lakini alipoulizwa kuhusu Mc Pilipili, Nicole alikataa kumuongelea huku akisema kuwa hakuna kitu chochote cha maana kitakachomfanya yeye amuonglee Mc Pilipili tofauti na Ery ambae wana bond ya kuwa na mtoto tayari katika maisha yao.
“Kitu kikubwa kilichonichosha kwa Mc Pilipili ni kujenga urafiki na baba wa mtoto wangu na kunisnitch” aliongea Nicole.Anaendelea kusema kuwa hata alipokuwa akiongea na Mc Pilipili kuhusu matatizo yake na Ery bado alikuwa anayafikisha kule kwa muhusika “thats was too bad na icho ndo kilichofanya nimemchukia”
Kwa Nicole , ni sawa kwa baba wa mtoto wake kuwa na urafiki na ex wake lakini sio mpaka wafikie hatua ya kumuongelea yeye,hata kama ni kwa faida zake lakini anakerwa na tabia ya ya Mc Pilipili kuingiza mambo yale katika urafiki wao.Nicole anasema kuwa kitu chochote kinachotokea kwake au Ery Kingu uwa wanaambia ndio maana ilikuwa rahisi kwake kujua.