“Mimi sina mpenzi” Ray C asema
Ingawa Ray C ni mrembo na mwanamke mwenye umbo la malkia bado hajaweza kuanza familia yake kwani hivi sasa hana mpenzi wala hana haraka ya kutafuta mtu wa kumpenda.
Muimbaji huyu amesema kuwa sasa hivi mawazo yake yote yako kwenye muziki na siyo mapenzi. Ray C ambaye alikuwa amepotelea kwenye madawa ya kulevya amejipa muda kufanya kazi yake ambayo aliiwacha baada ya haijakamilika baada ya kuzidiwa na raha ya madawa ya kulevya.
Hata hivyo akizungumza katika interview Ray C aliweza kusema kuwa hivi sasa anaonelea kuachilia nyimbo ambazo mashabiki wake watafurahia kabla ya kufikiria ikiwa atatafuta mpenzi wa kutulia na yeye. Alisema,
“Mimi sina mpenzi. Kwa sasa nafikiria kuhusu muziki wangu sitaki kujichanganya na mambo mengine. Mashabiki wangu wamenipambania kwa muda mrefu siyo kwaajili ya mpenzi wangu, wao wanataka kazi, muziki mzuri.”