“Mimi na Ruby Sio Marafiki” Nandy Atoa Povu Baada ya Ruby Kurudi THT
Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT, Nandy ametoa povu zito baada ya msanii mwenzake Ruby kutoka familia moja ya THT kurudi tena kwenye uongozi wake wa zamani.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa kuna mpambano mkali kati ya Ruby na Nandy kwenye kila kitu huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa wanafanana uimbaji wao na hata habari za wao kuwa na bifu kusambaa kila kona.
Hivi karibuni wawili hao walitudi kwenye vichwa vya habari na bifu lao krudi upyaa baada ya kupishana kauli ambapo Ruby apidai alipimzika kufanya mziki kwa muda wa mwaka mzimailo ampishe Nandy afanye mziki wake lakini Nandy alikana taarifa hizo na kudai kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka Ruby kukaa kimya ni nyimbo sake alizotoa kutokuvuma kutokana na ugomvi aliokuwa nao na management yake .
Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers Nandy alimwaga Povu lake kuhusiana na Ruby kurudi kwenye management yake ya zamani:
Labda ningeanza kwa kusema mimi na Ruby sio marafiki kila mtu anakuwa na marafiki zake ila kwa sababu wote tunatoka THT basi tunakuwa kama familia tukikutana tutaongea kuhusu muziki basi itaisha hivyo halafu sababu tu amerudi THT haimaanishi basi ndio niwe naye karibu ili niwafurahishe watu hapana mimi siko hivyo ikitokea Kama tutakuwa na ukaribu basi itakuwa hivyo na kama haitawezekana basi poa tu”.
Lakini pia Nandy amesema kuwa hana tatizo na kufanya kazi na Ruby kwa kuwa hivi sasa wote wapo THT endapo tu uongozi wake utaona kama ni vyema kwa biashara.