Mimi na Mume Wangu Hatugombani kwa Sababu Natambua Majukumu Yangu-Martha Mwaipaja

Msanii wa nyimbo za injili Tanzania martha mwaipaja amefunguka na kusema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakishindwa kutulia katika ndoa zao kwa sababu  wanakuwa hawatambui majukumu yao katika ndoa zao.

Martha anasema kuwa kila mtu anamajukumu yake katika maisha ya ndoa na jambo zuri ni pale ambapo watu hao wanakuwa wanaelewa majukumu yao na kuweza kuyatekeleza .akitolea mfano wa ndoa yake na mume wake , Martha anasema kuwa

download latest music    

mimi na mume wangu hatugombani kwa sababu natambua majukumu yangu kama mke, unajua  watu hawajui kuwa kiasili mungu amemuweka  mwanaume kuwa mtawala, amtawale mwanamke  sasa ugomvi mwingi unatokea  pale mwanamke anapotaka kuwa jeuri , kubishana na mwanaume”

Martha anasema kuwa jambo kubwa mwanamke anachotakiwa kujua ni kwamba mwanamke yuko chini ya mwanaume hivyo ugomvi mwingi katika ndoa utokea kwa sababu mwanamke anataka kuwa jeuri na kumbishia mwanaume.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.