“Mimi na Mke Wangu Amina Tunatarajia Kupata Mtoto Mwakani”-Ali Kiba
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Ali Salehe Kiba amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke Wake Amina Khaleef wanatarajia kupata Mtoto wao kwanza mwakani.
Baada ya fununu za muda mrefu hatimaye Ali Kiba ameweka wazi kuwa mke Wake Amina ni mjamzito na wanatarajia kupata Mtoto wao wa kwanza mwakani Baada ya kufunga ndoa mapema mwaka huu.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Radio Jambo ya Nchini Kenya alipokwenda kwa ajili ya kutangaza kinywaji chake cha MOFAYA , Ali Kiba alifunguka haya kuhusu ujauzito wa mke wake:
Katika dini yetu tunaamini ni faida kubwa ya ndoa Mtu kupata ujauzito, baada ya ndoa tu Mke wangu akapata baraka na Mungu akipenda mwakani tutabahatika kupata Mtoto, hatutajua ni Mtoto wa jinsia gani tunasubiria surprise, atakua Mtoto wangu wa nne”
Lakini pia Kiba ameweka wazi kuwa huyu atakuwa ni Mtoto Wake wa nne kwani tayari ana Watoto watatu na wanawake wengine aliowahi kuwa nao kwenye mahusiano siku za nyuma.