Mimi Mars Akiri Kuwa Ameshawahi Kuwa Mmbea Sana
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Marianne Mdee maarufu kama Mimi Mars amefunguka na kuweka wazi kuwa alivyokuwa Mtoto alikuwa na tabia za umbea.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mimi Mars ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Kodoo alisema zamani alikuwa na tabia ya kuongeaongea hovyo kiasi cha kuwakera wengi lakini anashukuru Mungu alivyokua hiyo tabia akaachana nayo.
Kweli ukiwa na utoto unakuwa na mambo mengi lakini ukikua unaacha, tabia yangu ya uropokaji na umbeya vilinifanya niogopwe. Yaani nikiwa nimekaa sehemu watu wananikwepa lakini najua ilikuwa utoto tu, sasa nimekuwa nimeacha“.
Mimi Mars ameongeza kuwa tabia hiyo ya umbea ilikuwa inamkera sana Dada yake staa wa Bongo fleva Vanessa Mdee kiasi ya kwamba walikuwa wanamtenga walipokuwa wanataka kuzungumza Mambo yao.