Mimba ya Agnes Bado Yamuumiza Kichwa Mbasha
Msanii wa nyimbo za injili, Mabasha bado anaandamwa na skendo ya kutembea na mwanamitindo Agness na kumpa ujauzito ingawa kwa nyakati tofauti msanii huyo amekuwa akikanusha wao kuwa na mahusiano nahata kumpa ujauzito mwanamitindo huyo.
Mbasha anasema kuwa yeye na agness hawajuani zaidi ya yeye kujua kuwa mwanamitindo huyo amekuwa kama shabiki yake na yeye amemjua kupitia mitandao ya kijamii tu.Mbasha amesema kuwa tetesi zinazosambaa juu yake hazina ukweli wowte na hawajawahi kuwa na ukaribu huo.
Agness namjua kama shabiki yangu kupitia kitandao ya kijamii tu,sasa sijui mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa kuwa mimi nina mahusiano nae.sijawahi kuwa na mahusiano na agnes wala kuwa na kitu chochote kinachoashiria mapenzi.
Sitegemei kupata nae mtoto kama watu wanavyosema kwa sababu sijawahi kuwa na mahusiano na mwanadada huyo,sina mahusiano nae huyo dada ni shabiki yangu tu.-Alisema Mbasha alipokuwa anaongea na Enews ya EATV.