Millen Magese Azidi Kuipa Sifa Tanzania Kimataifa.
Mwanadada Millen Happinese magese amekuwa ni mmoja kati ya icon kubwa ya Tanzania inayofanya vizuri nchi za nje kwa kufanya kazi zake kwa umakini lakini pia kuendelea kuitangaza vizuri Tanzania kwa kazi zake anazozifanya.Millen Magese aliwahi kuwa mshindi wa miss tanzania miaka ya 90 na kufanikiwa kuitangaza vizuri Tanzania katika mashindano ya u-miss Duniani.
Millen Magese amechaguliwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani katika chuo kikuu cha Havard kwa ajili ya kwenda kutoa hotuba juu ya ugonjwa wa Endometriosis ambao amekuwa akizunguka nchi mbalimbali kwa ajili ya kutoa uelewa wa ugonjwa huo.
Mwanadada huyo pamoja na kuendelea na kazi zake za kuwa mwanamitindo huku kazi zake akifanyia afrika ya kusini na marekani, amekuwa pia ni mmoja wa wanamitindo mashughuli na maarufu kwa kuwapa watu wengine uelewa juu ya ugonjwa wa endometriosiss na kusaidia baadhi ya wasichana katika baadhi ya nchi ikiwemo tanzania ambapo alikuwa na nia ya kutoa matibabu ya ugonjwa huo kwa wasichana wenye umri mdogo kabla ugonjwa huo haujakomaa na kusababisha matatizo makubwa ya upatikanaji wa mtoto.
Ugonjwa huo ambao pia ulimsumbua Millen kwa muda mrefu , lakini aliweza kupambana nao hata kupata matumaini ingawa ugonjwa huo unakuwa na dalili kubwa ya kutopata mtoto lakini kwa Millen hakukata tamaa kwa sababu wakati akihamasisha wengine kusaidia na kuuelewa ugonjwa huu lakini pia alikuwa akifanya jitihada za kutafuta mtoto.Ambapo ushindi wake unakuja pale baada ya kupitia magumu ya muda mrefu alkini alikuja kuonekana kuwa shujaa baada ya kupata mtoto wake wa kwanza wa kiume mwaka uliopita.