Mike Adai Kuwa Hataki Hata Kusikia Suala La Ndoa
Msanii wa filamu za Bongo movie Mike Sangu amefunguka na kusema wazi wazi kuwa hataki hata kusikia Suala kufunga ndoa kwa muda mrefu sana.
Mike amesema kuwa sio kwamba haoni wanawake wa kuoa tangu atengane na mkewe msanii mwenzake wa Bongo movie, Salome Urassa ‘Thea’ bali hana hamu na ndoa tena kwani imemkinahi.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mike alisema kuwa anakutana na wanawake wengi ambao angetaka kuingia nao kwenye ndoa asingeshindwa lakini wito wa kuoa umepotea moyoni mwake.
Kiukweli sina hamu ya kuoa tena mpaka moyo wangu utakapokubali, ni kama ndoa imenikinahi hivi na si kwamba sina wa kuwaoa, wapo wengi lakini bado siko tayari“.
Mike na Thea waliachana miaka kadhaa ya nyuma ambapo walikuwa bonge la varangati na kuanika mambo yao katika magazeti ya udaku.