Mh Shonza Azungumzia wimbo wa Tetema.
Mh naibu waziri wa sanaa na michezo julina ashonza amefunguka na kuzungumzia wimbo mpya wa Diamond pamoja na rayvany .Mh julina anasema kuwa ameufurahia wimbo huo na kuwa wamejitahidi sana kuuweka wimbo huo katika maadili yanayotakiwa sio kama inavyokuwa katika nyimbo hizo.
hata hivyo , alipokuwa akiongea na Wasafi Tv, mh shonza anasema kuwa ameuona wimbo ni mzuri na aliamini kuwa utakuwa mzuri kwa sababu diamond platinumz amekuwa akijitahidi kufanya vizuri na pia ni mwanamke mzuri.
Wimbo wa tetema ni moja ya wimbo ambao kwa wasanii hawa kutoka WCB hawakusumbuliwa kuurekebisha kwa namna yoyote kama nyimbo ambazo zimepita hapo nyumbani kutokana na kuzoeleka kwa wasanii hawa kutoa nyimbo ambazo zinakuwa na uvunjaji wa maadili kama ule uliopita wa mwanza.