Mh.Nape akanusha kushindwa kuwapatanisha Diamond na Alikiba
Aliyekuwa waziri wa habari na michezo ambae pia ni mbunge wa Mtama kupitia chama cha CCM mh.Nape Nnauye amefunguka kuhusu jitihaada zake za kutaka kuwapatanisha wasanii wakubwa nchini Diamond na Alikiba kipindi cha uongozi wake katika sekta hiyo ya michezo,mh. nnauye anasema kuwa sio kweli kuwa alishindwa kuwapatanisha ila jitihada hizo zilikwama kutokana na uongozi wake kukoma ghafla, kwa sababu ambayo iko wazi.
Mh.nape alipokuwa waziri wa habari na michezo alikuwa ameunda kamati iliyowashirikisha wasanii hao ili kuchangia vijana wa mpira wa miguu,kamati iyo ilikuwa na lengo la kuwakutanisha diamond pamoja na alikiba pamoja ili kufanya kampeni za kuhamasisha wananchi kuchangia kusaidia timu ya Taifa ya Serengeti boys under 17 ambao walikuwa wanaenda kucheza nje ya nchi,Mh. nape anasema kuwa lengo kubwa ilikuwa ni kuweka historia ya kuwafanya Diamond na alikiba kuwa na wimbo ulioimbwa pamoja hata kama hawatakutana sehemu moja yaan katika wimbo huo kila mtu awe na verse yake katiaka wimbo huo,katika kuwaunganisha huko walishatengeneza na beat ,ilikuwa ni swala la muda wa kuwakutanisha tu ili kutengeneza wimbo.
Kiongozi huyo anasema kuwa bifu la Diamond na alikiba ni zuri endapo msuguano wao utakuwa mzuri kama utakuwa na manufaa ya kukuza muziki nchini , kama mmoja anatoa wimbo huu na mwingine akatoa huu ni vizuri pia kama ilivyo sasa mmoja ametoa seduce me mwingine katoa zilipendwa, anaongezea kwa kutoa mfano wa uwepo wa wasanii wa zamani wa taarabu kama khadija kopa na Nasma Kidogo ambao walikuwa wanapigana vijembe lakini walikuwa wananogesha sana muziki wa taarabu kutokana na ushindani wao katika muziki huo .
Mh. Nape alifananisha bifu la diamond na alikiba kama ushindani wa simba na yanga ‘leo ukitaka mpira ufe basi ua bifu la simba na yanga , ukishaliua tu na mpira unakufa , hivyo ndio burudani ilivyo ‘ anaongezea kuwa kama bifu liwepo ila tu lisivuke mipaka ya kujenga chuki na kutaka kuumizana.