Mensen:Mama Alifia Mikononi Mwa Pam D

Msanii wa muziki wa kizazi kipya ambae pia ni producer wa nyimbo za kibongo Mensen Selekta  amefiwa na mama yake mzazi siku ya KrismasA baada ya kusherekea sikukuu hiyo na baadae hali yake kuanza kubadilika na walipompeleka hospitali mama huyo aliaga Dunia hapohapo.

akiongea na GPL Mensen alithibitisha kufiwa na mama yake mzazi siku ya Jumatatau ambayo ilikuwa siku ya krismas baada ya ya kuzidiwa kutokana na maradhi ya kisukari aliyokuwa nayo kwa muda mrefu,Mensen anasema kuwa mama yake alishinda vizuri siku nzima lakini baadae jioni alianza kujisikia vibaya ndipo walipomkimbiza hospitali lakini kwa bahati mbaya walishindwa kuokoa maisha yake.

download latest music    

Nimeumia sana mama yangu amefariki Jumatatu tulipokuwa hospitali, alifariki mikononi mwa binamu yangu Pam D.Tunategemea kusafirisha siku ya alhamisi kwenda Tanga kwa ajili ya mazishi.

GPL iliamua kumtafuta Pam D ambae inasemekana kuwa alikuwepo siku ya tukio, na alithibitisha hilo na kusema kuwa shangazi yake alifariki siku hiyo baada ya kubanwa na kifua kwa muda na kisha kukutwa na umauti.

Tunatoa pole kwa Mensen Selekta, Pam D na familia kwa kipindi hiki kigumu cha kupotelewa na mpendwa wao.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.