Menina- “Kuzaa Kulinipoteza Kwenye Bongo Fleva ”.
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Meninah Atik ambaye alijizolea umaarufu Baada ya kushiriki kwenye mashindano ya Bongo Star Search mwaka 2012 ametangaza kurudi kwenye gemu rasmi.
Meninah ambaye katika miaka michache iliyopita ameolewa ndoa mbili na sasa amejaaliwa kuzaa Mtoto Wake wa kiume ambaye kwa sasa ana umri wa mwaka mmoja.
Menina ametangaza kurudi rasmi kwenye muziki Baada ya kimya cha miaka kadhaa.
Katika mahojiano yake na Global Publishers, Meninah alisema kwenye ulezi kuna mambo mengi hivyo ilikuwa lazima atulie ili amlee mtoto kwanza.
Ulezi una kazi sana hivyo niliamua kulea kwanza, lakini mpaka sasa niko vizuri siku si nyingi mashabiki wangu watanisikia tena kama kawaida”.