Meneja Wa Harmonize Afunguka Kuitosa WCB
Meneja wa staa wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB, Harmonize anayejulikana kama Mr. Puaz amethibitisha kuachana na Harmonize kwa like alichodai ni kukosa maelewano.
Licha ya Harmonize kuwa chini ya WCB Lakini pamoja na wasanii wengine wa label hiyo wana mameneja tofauti ambao wanasimamia kazi zao.
Kwenye mahojiano na Gazeti la Risasi la Mchanganyiko, Mr. Puaz alikiri kuacha kufanya kazi kama Meneja wa msanii huyo Lakini amekana kuwa na Bifu na msanii huyo wala Label ya WCB.
Ni kweli kwa sasa mimi na Harmonize hatufanyi kazi pamoja kwa sababu ya kupishana kauli; lakini haimaanishi mimi na WCB hatufanyi kazi au hatutafanya kazi.
WCB ni familia yangu ambayo ukaribu wangu na wao ulitokana na urafiki wangu na Diamond hivyo siwezi kuiacha, panapo kuwa na nafasi ya mimi kuhitajika kutoa mchango wangu nitaendelea kutoa kama mwanafamilia“.