Mdogo Wa Ndikumana Kuiponda Bongo Movies
Mdogo wak maraehem Hamad Ndikumana anajulikana kama Laddy Ndikumana amefunguka na kuwatukana wasanii wa bongo movies kwa kuwaita wanafiki kutokana na kutoonekana katika msiba wa kaka yake wakati kipindi yupo hai wengi walikuwa wakionekana kuwa karibu nae
Hamad Ndikumana ambae alikuwa mume wa msanii Irene Uwoya awa ndoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja alifariki wiki iliyopita kwa ugonjwa wa moyo na kuzikwa huku kwao nchin Rwanda.Irene Uwoya alifanikiwa kwenda kuzuru karibu la mzazi mwenzie huyo ingawa hakupata bahati ya kuzika mwili wa marehemu.
Akiongea na Big Chawa wa Planet Bongo ya East Afrika Laddy Ndikumana alisema kuwa wasanii hao wamekuwa wajinga na wanafiki sana kwa kuwa wameshindwa kufika katika msiba wakati kipindi yupo hai wengi walikuwa marafiki zake na walikuwa karibu nae kwa kipindi chote.laddy anasema kuwa kipindi kaka yake alipokwa na hela walikuwa wanakula nae bata kila kukicha.
Wapo baadhi ya wasanii walionyeshwa kuguswa na msiba huo na kufika nyumbani kwa Irene ambapo familia ya mwanadada huyo ilikuwa ikiombeleza msiba huo kabla ya kupanga safari ya kwenda rwanda kwa ajili ya mazishi ya mwanasoka huyo ingawa hawakuweza kuwahi, hata hivyo wapo baadhi ya watu kutoka bongo movies ambao waliongozana na mwanadada Irene katika kuhani msiba huo akiwepo Mike Sangu ambae alitumwa kama mwakilishi wa bongo movies.