Mdogo wa Alikiba Katika Penzi Nzito na Star wa Taifa Stars
Ndugu wa kike wa msaini alikiba , Zabibu Kiba amejikuta katika penzi zito na mchezaji wa mpira nchini tanzania kutoka katika timu kubwa nchi ya Taifa Star anaejulikana kama Abdi Banda .katika ukurasa wake wa instagram , mcheza mpira huyo amekuwa akimpost na kuweka picha za mwanadada huyo mara kwa mara na hata kufanya watu waanze kuingilia mahusiano yao kwa kuwasahauri kuoana kabisa.
Abdi Banda mchezaji wa Taifa Stars.
Kwa muda mrefu haikuwahi kufahamika mtu wa karibu wa mwanadada huyo lakini kadri siku inavyozidi kwenda mambo yanazidi kuwa mambo kwa sababu mapenzi ni kama kikohozi huwa hayajifichi kabisa.
Katika siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mwanadada huyo, Star huyo aliandika na kuweka picha yake kwa ajili ya kumatakia kheri ya siku hiyo ya kuzaliwa kwake.