Mbunifu wa Mitindo Nchini Aalikwa na Malkia wa Uingereza.
Mbunifu wa mitindo nchini ambae amekuwa akifanya kazi ya ubunifu wa mitindo kwa muda mrefu na anaweza kusema kuwa ni moja ya wasanii wakongwe ambao walikuwa wanainua vipaji vya mitindo nchi Mustafa Hassanali amealikwa na Malkia wa Uingereza ambapo kutakuwa na sherehe kubwa nchini Uingereza itakaojumuisha watu mbalimbali na yeye akiwa ni mmoja ya wanamitindo wanaotoka katika nchi za Jumuiya ya Madola..
akiongea kuwa furaha na heshima kubwa hassanali anasema kuwa kwake ni heshima kubbwa kwa sababu ni sherehe ya kifahari inayoenda kufanyika huko hivyo hiyo itampa fursa yeye na kuitangaza tanzania nchini humo.
Ni heshima kubwa sana na ufahari kualikwa na Malkia katika sherehe ya kifahari kama hiyo inayoenda kufanyika katika hekalu la Buckingham kwa mari ya malkia kuweza kusherekea nae na kazi za mitindo kutoka nchi zote za jumuia ya madola, hii inaonyesha kuwa kazi yako ya kujitolea katika sekta ya mitindo ya tanzania inakubaliwa na kutambuliwa kimataifa.
Ninachoshukuru ni kwamba kwa miaka mini nimekuwa nikileta mabadiliko katik tasnia ya mitindo , nimeleta mabadiliko mabayo nilitamani kuyaona katika sekta ya mitindo ya hapa nchini, kama raisi wa marekani alivywahi kusema kuwa uisulize nchi yako imekufanyia nini ila jiulize umeifanyia nini nchi yako.
Hii ni heshima kubwa sana kwa nchi na kwa mwanamitindo huyu kwa sababu fursa hii inato nafasi ya mwanamitindo huyo kuonana na kukutana na watu tofauti wanaoenda kusherekea katika sherehe hiyo.