Mbosso Amefungukia Tetesi za Kushindana Kimuziki na Aslay

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Marombosso au Mbosso anayeendelea kufanya vizuri na wimbo wake wa ‘ kiben10’ Amefungukia habari za Bifu na ushindani uliopo kati yake na msanii mwenzake Aslay.

Mbosso na Aslay walikuwa kwenye kundi moja pamoja na Enoch Bella na Beka, kundi lililojulikana kama Yamoto Band lililojipatia umaarufu miaka ya nyuma kutokana na nyimbo zao kali na staili zao tofauti katika uimbaji lakini baadae kundi hilo liliishia kivunjika.

download latest music    

Baada ya kundi hilo kuvunjika na wasanii kutengana kila msanii alianza kufanya mziki kivyake kama solo artists na mara moja Aslay alianza kung’aa kivyake na kuanza kupata mafanikio ya haraka kuliko wenzake wote aliokuwa nao.

Mara baada ya kuwa mwenyewe Aslay alianza kutoa nyimbo nyingi mara kadhaa na kila nyimbo anayotoa zimekuwa zikishika namba moja kwenye chati mbali mbali jambo lililofanya akajizolea umaarufu mkubwa.

Lakini kama ilivyo kwa Aslay Mbosso naye akiwa msanii anayejitegemea alisainiwa chini ya label maarufu zaidi Tanzania inayosimamia masupastaa kama Diamond, Rayvanny, Harmonize na wengineo wengi.

Lakini mara tu baada ya Mbosso kusainiwa na WCB kumekuwa na tetesi za kuoneana Wivu na kufikia hatua ya kushindana wenyewe kwa wenyewe tuhuma ambazo Mbosso amezikataa na kusema hana wivu na Aslay na pia hawezi kushindana naye:

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni Mbosso alifunguka haya kuhusu uhusiano wake na Aslay:

Mimi naheshimu mziki wa Aslay kwa sababu ni mtu ambaye nimemkuta kwenye Industry halafu kwangu mimi yule ni brother namheshimu na yeye ananiheshimu sana yaani tunaheshimiana”.

Mbosso amekuwa akifanya vizuri sana tangu ajiunge na WCB ambapo nyimbo zake kiben10 na Watakubali zote zinafanya vyema lakini pia wasanii wote waliounda kundi la Yamoto wanafanya vizuri kama Beka na Enock Bella.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.