Mbasha Akanusha Tetesi za Kutoka na Agness Mmassy
Msanii wa nyimbo za injili emmanuel mbasha amefunguka na kuamua kuweka wazi mahusiano yake na mwanamitindo maarufu nchini agnes mmasi na kusema kuwa watuwamekuwa wakizusha kuusu yeye kutoka kimapezni na mwanadada huyo lakini taarifa hizo sio za kweli.
atika UkIrasa wake wa instagram , Mbasha aliandika “Nakanusha yote ni uongo, sia mahusiano na huyu dada kabisa na wanaoendelea kuzusha na kueneza huu uongo basi na mungu wangu atawalipa.sio kweli.”
Kumekuwa na tetesi katika mitandao ya kijamii kuhusu mahusiano kati ya mwimbaji huyo na mwanadada mabe ni mwanamitindo ambae amekuwa akipiga picha za utupu mara nyingi na kuziweka katika mitandao ya kijamii Agness Mmasy.
Hata hivyo kwa rekodi ya hivi karibuni, Emmanuel Mbasha alikiri kutokuwa na mwanamke tangu alipoachana na mke wake Florah na kusema kuwa kwa sasa hivi amejukita zaidi katika swala la uokovu na kwamba kuwa na mahusiano kabla ya ndoa ni kuzini na asingependa kufanya kitu hicho.