Mavoko- Sina Tatizo na WCB, Niko Tayari Kupiga Nao Kazi
Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Richard Martini maarufu kama Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa hana tatizo kabisa na uongozi wake wa zamani WCB.
Miezi michache iliyopita Rich Mavoko alitangaza Rasmi kujiengua Kwenye Label ya WCB alipokuwepo kwa miaka kadhaa kutokana na matatizo ya Kimkataba.
Leo hii Rich Mavoko yupo chini ya uongozi mpya ambao hajauweka wazi Lakini pia ameachia nyimbo zake kadhaa kama Ndegele, Hongera, Naogopa na Navumilia.
Kwenye mahojiano na Global Publishers, Mavoko amefunguka na kuweka wazi kuwa pamoja na kuondoka WCB lakini hana tatizo nao:
Unajua watu wengi wanashindwa kuelewa, sikuondoka WCB kwa ugomvi kule hata kidogo ni mambo tu ya kawaida ya kimuziki lakini sina tatizo na yeyote yule”.
Lakini pia Mavoko ameweka wazi kuwa kama itatokea WCB watakuwa tayari kufanya naye kazi hivi sasa basi yeye hana tatizo:
Sina tatizo kabisa, tutakaa chini na kuzungumza si ni biashara tu?”.