Maua Sama Haogopi Nafasi ya Iokote Kutambulisha Wimbo Mpya.
Mwanadada Maua sama anasema kuwa katika maisha yake ya muziki kwa sasa pamoja na kwama wimbo wake wa Iokote ni wimbo ulifanya kazi vizuri sana kwa mwaka huu lakini bado anaona kuwa sio kitu yeye kuogopa kufanya wimbo mwingine akihofia nafasi ya ule uliopita.
Maua anasema kuwa hataki kusumbuliwa na presha ya Iokote kwa sababu hata wakati anatoa wimbo huo hakuwa amefikiria kama utachukua nafasi kubwa kiasi hicho.
Maua Sama anasema ” Unajua wasanii wengine wamekuwa wakipotea kwa sababu ya kufanansiah nafasi ya wimbo waliotoa na ule uliopita, lakini kwangu ni tofauti kwa sababu tayari nimeshajianda kuja na muziki wangu ambao ni kawaida kuwakonga nafsi za mashabiki.”
Maua anasema kuwa hakuna wimbo ambao aliona anaweza kukosea kama wimbo wa iokote kwa sababu haikuwa style yake ya muziki lakini ndio umefanya vizuri mpaka anashangaa.