Matukio ya Kupokea na Kuaga Mwili wa Marehemu Ruge jijini Dar Es Salam
Mwili wa Marehemu Ruge Mutahaba Uliwasili siku ya Ijumaa na kupita maeneno mbalimbali ya Jiji la Dar Es Salaam na baade kupelekwa katika hospitali ya Lugalo.
Siku ya jumamosi , ulipelkwa katika viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuagwa na watu mbalimbali na kuupatia heshima za mwisho kabla ya kusafirishwa na kupelekwa kijijini kwao BUKOBA ambapo ndipo mwili huo utazikwa katika nyumba yake ya milele.
Ruge ameliza wengi na wengi wameumia na msiba huo , huku kila mmoja aamini kwa jinsi watu walivyojitokeza kwa ajili ya kuupokea na kuupoa heshima zake za mwisho kwa DAR na hata ulipofika kwao BUKOBA.
Mwili wa Ruge ukiwasili na kushushwa Uwanja wa Taifa.
Mwili wa marehemu ukipita katika maeneo mbalimbali ya Jijini Dar.
jeneza la marehemu likiwa limewasili viwanja vya karimjee tayari kwa kuagwa.
Familia ya marehemu (watoto wake na wazazi wenzake na Ruge) wakiwa katika ukumbi wa Karimjee.
Mh Magufuli akitoa mkoo wa pole kwa wazazi wa marehemu.
Baadhi ya wasanii wa THT wakiwa katika majonzi wakiimba Nyimbo za kuombeleza.
Nandy ni moja ya wasanii waliopata fursa ya kuimba wimbo aliokuwa akiupenda marehemu lakini alishindwa kuendelea na mtoto wa marehemu alimsaidia kushuka jukwaani.
Barnaba alipokuwa akiongea machache kuhusu baba yake Ruge na baada ya hapo alishindwa kuendelea na kuzimia.
Zamaradi mketema ambae ni mzazi mwenza na Ruge akiingia uwanjani hapo.
Baadhi ya wasanii wakiwa katika viwanja vya karimjee kwa ajili ya kuaga mwili wa Marehemu.
Baadhi ya watu siku ya jumapili wakisubiri mwili wa marehemu Ruge kuwasili katika viwanja vya ndege BUKOBA.