Matukio Makubwa Yaliyotikisa Mwaka 2017, Upande Wa Burudani.

Kila kitu kina historia Duniani, pia kwa upande wa burudani Tanzania kuna matukio makubwa yaliyotokea ambayo utakapo wauliza wahusiaka lazima watakwambia kuwa hawawezi kusahau swala hilo.

Lulu Kufungwa Jela.

download latest music    

Mnamo tarehe 13 November, mwanadada mrembo kutoka bongo movies, alipokea kifungo chake cha kutumikia miaka miwili gerezani baaba ya kukutwa na hatia ya kuuua bila kukusudia.Kesi hiyo ya mauaji ilitokea mwak 2012 baada ya Lulu na aliyekuwa mpenzi wake Kanumba kugombana na kusababisha umauti wa mwanaume huyo.

Tukio ilo lilitikisa Tanzania nzima hasa wapenzi wa sanaa , kwa sababu wengi walikuwa wakimpenda Lulu na kazi zake pia.

 

Kutekwa Kwa Roma  na Wenzake.

usiku wa april 26, wasanii wawili roma mkatoliki na moni centrozone walitekwa na kwenda kusikojulikana huku kukiwa na kigugumizi cha kutokujua wapi walipokuwa.baada ya kupotea kwa wasanii hao wasanii wengi waliungana kwa pamoja na kuanzisha kampeni ya ‘Free Roma’ ili kumsaidia mkewe na familia kujua wapi alipo.

kama baada ya siku 3, roma na wenzake waliachi wa huru na watekaji hao huku wakiwa na majeraha mengi katika miili yao, cha ajabu na kushangaza hakuna anaejua siri ya kutekwa kwao mpaka sasa kwa sababu msanii huyo hakutaka kulizungumzia hilo.

Babu Seya   na Papi Kocha kutoka gerezanai.

Tarehe 9 Desemba mwaka huu Rais Magufuli aliweka tena historia kwa kitendo cha kuwatoa na kuwapa uhuru  wasanii wakongwe Babu Seya na Papi Kocha, hii ilikuwa ndoto ya wasanii na wananchi wengi kutokana na maombi ya wasanii hao kutoka.Tarehe hiyo ilikuwa ni moja ya siku kubwa na yenye furaha sana kwa watanzania wengi sana baada ya wasanii hao wakongwe kutoka.

Hamisa kuzaa na diamond Platinumz

Timbwili lilianza pale ambapoa hamisa alianza kusema kuwa ana mahusiano na msanii mkubwa Tanzania Diamond Platinumz ambapo Diamond alikana taarifa hizo lakini baadae Hamisa alijulikana kuwa ni mjamzito na kufanya watu kaamini kitendo hicho lakini kwa Diamond mwenyewe ilikuwa tofauti kwa sababu alikana katika vyombo vya habari na kusema mimba ya Hamisa sio ya kwake.Hamisa aliamau kuvujisha picha za mahusiano yake na Diamond na kufanya mtandao wa instagram kuzizima na hatimaye Diamond aliamua kuweka wazi na kukubali taarifa hizo katika vyombo vya habari na kuiomba radhi familia yake.

Wasanii na kashfa za madawa ya kulevya

Mh.Makonda  aliibuka na kuanza kupiga vita ya madawa ya kulevya ambapo wasanii wengi walizolewa na kusweka Lumande .Hakuna aliyetegema kuwa wasanii wakubwa na wanaopendwa wanaweza kuwa katika list ya watumiaji wa madawa ya kulevya.Wasanii kama Wema Sepetu, TID, Vannesa Mdee, Mr Blue, Lulu Diva,Tunda na Rommy Jones.Ambapo baada ya kesi na mahojiano, Agness Masogange walikutwa na hatia na mpaka sasa kesi zao ziko mahakamani.

Swala la Wema  Sepetu na vyama vya siasa.

tarehe 24 february wema sepetu aliahama kutoka CCM kwenda CHADEMA, hii ni moja ya headline kubwa katika vyombo vya habari kwa mwaka huu.hii ilitokea siku chache baada ya wema kutajwa kuwa katika list ya wasanii waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya.

Lakini tena Deseba 1 , mwaka huu huu tena wema sepetu alitangaza kuhamia kutoka CHADEMA na kurudi tena CCM.

Ndoa ya Irene Uwoya na Dogo Janja

Hii i moja ya mambo yaliyowaacha watu maneno ya kuongea sana katika mitandao ya kijamii, irene uwoya na Dogo janja walifunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu.Watu wengi walishangaa kutokana na umri wa Dogo Janja kuwa mdogo zaidi ya mwanamke aliyemuoa.

Penzi la Jux na Vannesa Mdee.

Vannesa Mdee na Jux waliingia katika trending ya mitandaoni mwaka huu baada ya kuwa moja ya couple nzuri na pendwa Tanzania kwa upande wa wasanii, lakini baadae hakuna sababu iliyokuwa wazi ambayo ilisababisha wawili hao kuachana, mashabiki wao walipiga kelele sna na kutaka warudiane.Tamasha kubwa la FIESTA linalozunguka karibia kila mikoa liliwafanya wawili hao kurudiana na kuendelea na mapenzi yao mwishoni mwa mwezi November.

 

 

 

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.