‘Mastaa Wengi Wanataka Mapenzi Ya Kweli na Sio Pesa”- Esther Kiama
Msanii wa filamu za Bongo movie Esther Kiama ameibuka na kusema kuwa mapedeshee wa mjini hivi sasa hawana dili kama zamani kwani wasanii wengi wa kike hawaangalii pesa bali wanataka mapenzi ya kweli.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Ester alisema mastaa wengi wamegundua mapenzi ya kweli hayapo kwa mapedeshee ambao walikuwa wanawatumia tu kupitia hela zao.
Unajua zamani mapedeshee walikuwa wakitumia mifuko yao kuwarubuni mastaa mbalimbali lakini sasa mambo yamebadilika, wengi wa wasichana sasa hawatazami pesa bali mapenzi ya kweli na ndio maana ukichunguza utaona mastaa wanatoka na wanaume wa kawaida sana ambapo wakati mwingine si rahisi kuamini“.
Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakitajwa kuwa na mahusiano na wanaume wenye pesa wanaojulikana kama mapedeshee.