Mastaa Wanaoficha Watoto Wataumbuka: Shilole

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na mfanyabiashara maarufu Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole amefunguka na kusema wasanii wanaoficha watoto watakuja kuumbuka.

Maneno hayo yamesemwa mara baada ya sakata la Msanii Muna Love kutawala vichwa vya habari baada ya kudaiwa kumtelekeza mtoto wake wa kumzaa mwenyewe.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Shilole amesema hakuna siri duniani na wasanii wa kike ambao wamekuwa wakiwaficha watoto wao na kusema hawajawahi kuzaa au walizaa wakafa, ipo siku wataumbuka, pia wanatakiwa kutambua kuwa wanakosa riziki kwa sababu ya kuwaficha malaika hao wa Mungu.

Hakuna siri duniani, ipo siku Mungu atawaumbua wote wanaodanganya kwamba hawana watoto au wamekufa, kuficha malaika hao wanakosa riziki ambazo wangepata kupitia wao, jamani wanawake wenzangu badilikeni, kuwa na mtoto au watoto siyo kashfa ni baraka maana wapo wanaotafuta wanakosa“.

Shilole amekuwa mmoja kati ya wasanii ambao wameweka wazi kukerwa na baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakifanywa na Muna kuanzia msiba wa mtoto wake Patrick mpaka sakata lake la kumkataa mtoto.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.