Mastaa Wa Kike Maarufu Na Muonekano Wa Nywele Fupi
Imekuwa fashion kwa wanadada wengi kuwa na muonekano wa nywele fupi , tena wakionekana maridadi kabisa kuliko hata nywele za bandia wanazosuka wakati mwingine.Hawa ni baadhi ya mastaa na watu maarufu wa kike bongo wenye muonekano wa nywele fupi na bado wanaonekana maridadi na kupendeza vizuri kabisa.
1.Nancy sumary.
Amekuwa akionekana na muonekano huu kwa muda mrefu sasa, ni mwanadada mjasirimali, muandishi wa vitabu lakini pia ni meneja wa Bongo5 Media.Ni mama wa familia lakini muonekano wake siku zote umfanya kuonekana mrembo bila kuchuja.
2.Elizabeth Lulu Michael
Amekuwa na muonekano wa kubadilika badilika katika nywele , lakini akiwa na nywele fupi uonekana vizuri zaid.ni mmmoja wa mastaa wa bongo movies anaeongozwa kwa kupendeza na kuvaa nguo ikamkaa vizuri kabisa.Huyu ndio Lulu Michael.
3.Jackline wolper
Jacky ni mmoja wa wasichana wanaovaa sana katika mastaa wa bongo, amekuwa ni mtu anaejipenda.Kuwa na duka la mavazi pia linazidi kumfanya aonekane maridadi.yeye pia anamuonekeano wa nywele fupi ila za kwake amezitia nakshi, hii inamfanya azidi kung’ara kwa sababu ya rangi yake pia.
3.Faraja Nyalandu
Ingawa ni muda sasa tangu ashiriki mashindano ya ulimwende, lakini amekuwa ni mmoja wa wanawake wanaotunza umaridadi wao sana.Akiwa kama mama wa familia pia Faraja amekuwa akivaa nguo za heshima, zenye kumfanya haonekane binti muda wote na kuonekana nadhifu na muonekano wake wa nywele fupi.She is always perfect!!!!!
5.Jackline Ntuyabaliwe
Ni moja wa mwanadada mwenye vipaji vingi, alianza na urembo, baadae akaingia kwenye muziki lakini sasa amejikita katika ubunifu zaidi na kampuni yake ya kutengeza vitu vya thamani chini ya kampuni ya Amorette.amekuwa na muonekano mzuri sana hasa katika nywele fupi. Huvaa simple but always looks stunning!!!
6.Shamimu Mwasha(8020 Fashion)
Inawezekana labda na kazi yake inamfanya aonekane maridani zaidi, amekuwa mwanamitindo na pia mtu ameweza kushauri wengine na kutoka kimaisha.shamimu ni mama wa familia,Mwanamitindo na mjasiriamali pia lakini hii haifanyi yeye kuonekana toauti na wasichana warembo na wanaojipenda.