Mashindano Ya Miss Tanzania Kutofanyika Tena
Kumekuwa na taarifa zisizoeleweka kuhusu shindano la miss tanzania mwaka huu kufa nyika au kutokufanyika kabisa, mara ya kwanza ilisemekana kuwa bado wanarafura wadhamini amabo watakuwa wanatoa ahadi za ukweli kwa washuindi wanaposhinda kwa sababu mwaka uliopita mshindi wa Miss Tanzalia aliangaika sana mpaka kupata zawadi zake na hata hivyo kuba baadhi ya zawadi hakuzipata kabisa.
Limekuwa ni moja ya jambo la kusua sua kwa fainali ya Miss Tanzania kufanyika wakati huko mikoani na katika ngazi ndogondogo jambo hilo linafanikiwa, lakini sasa hii itaweza kuwa labda ni taarifa rasmi kuwa mashindano hayo hayatakuwepo kwa mwaka huu , sijui kwa miaka ijayo lakini kwa sasa wadhamini wamekosekana wa kuendesha mashindano hayo.
Waandaaji wa urembo wa Miss Tanzania kampuni ya Limo Internatinali Agency wamesema kuwa hakutakuwa na fainali ya mashindano ya urembo kwa mwaka huu 2017.Kampuni hiyo imesema kuwa sababu kubwa ya kutokuwepo kwa fainali ya mashindano hayo ni kwa sababu hakujapatikana kwa wadhamini watakaodhamini shindano hilo na kutoa zawadi kwa washindi.
Hata hivyo kampuni hiyo imesema Kuwa kulikuwa na ucheleweshwaji wa kupatikana kwa kibali cha kuendesha shindano hilo la Miss Tanzani amabcho huwa kinatoaka BASATA ambapo kibali hicho kilitolewa mwezi Septemba na kuwafanya kushindwa kujiandaa kwa vitu vingi ikiwemo hiyo ya kushindwa kutafuta wadhamini hao.
Ikumbukwe kwamba mapema mwaka huu Tanzania ilitakiwa kutoa mshiriki mmoja kwenda kushiriki Miss World lakini kwa sababu mashindano hayo yalikuwa hayajafanyika ilibidi kuteua mshiriki wa pili wa mwaka jana ili kuwakirisha Tanzania.
Shindano la Miss Tanzania limekuwa likifanyika kila mwaka na kuibua warembo ambao wamekuwa ni mchango mkubwa katika tasnia ya urembo na uchumi wa ndani na nje pia akiwepo Wema Sepetu, Jokate Mwegelo, Nancy Sumary,, Faraja Nyarandu na wengine wengi.