Mashabiki Waingilia Kati Penzi la Diamond na Zari
Wakati Diamond mwenyewe akiwa amekaa kimya hataki kuongelea mahusiano yake na mzazi mwenzie tangu mwanamke huyo aliposema rasmi kuwa ameachana na Diamond na kisha kufanya mahojiano katika chombo kikubwa cha habari Duniani, mashabiki wa pande zote mbili wameonekana kukerwa na kuhuzunishwa sana na kuachana kwa wawili hao huku wakijitahidi kutoa ushauri kwa pande zote mbili kwamba wanataka wawaone wakiwa pamoja.
Katika mitandao ya instagram imekuwa ni kama desturi kukuta kuwa karibia kila picha inayowekwa na zari au diamond ni lazima itaongelea mahusiano yao ya kimapenzi kutoka kwa mashabiki wao.Wapo wanaoongea maneno makali kuonyesha kuwa na hasira kwa kuvunjika kwa penzi hilo na pia wapo wanaoonekana kuwa na hisia za huzuni kwa wote wawili na watoto wao pia.
amuru tanzania
please shemeji zarimond do not hesitate to say no with big no,learn to say no in a small letter.go back to your gentleman.
mrlv3462
u look so pretty ila unapendeza sana ukiwa na baba watoto wako mond.
sihakaadam
acha ujinga wewe rudi kwa mwenzako muelewane na muleee watoto wenu , mimi ninaamini kuwa wanaume unawajua vizuri tu…cha msingi piga moyo konde na urudi kwa mwenzio.musiwape maneno wapambe nuksi.
tiritendebe
mamy naomba umsamehe jamani
paulinafaustine
Zari maisha ni safari ndefu jamani,jaribu kutuliza akili yako na utafakari hata wazazi wetu walipitia mapito hayohayo lakini walivumilia mpaka hapo walipofika , kwaio maisha ya ndoa yana misuko suko kwaio piga moyo konde.
Zari na Diamond waligombana na kufikia maamuzi aliyotamka zari baada ya kuchoka kupokea skendo za mzazi mwenzie kuwa na wanawake kila siku huku sababu kubwa iliyomuumiza zari ni ukaribu wa Wema sepetu na Diamond ulioanza hivi karibuni.