Martin Kadinda Amkana Wema Sepetu
Mbunifu wa mavazi Tanzania na aliyekuwa meneja wa staa wa Bongo movie Wema Sepetu, Martin Kadinda amedaiwa kumkana Wema baada ya kuulizwa kuhusu uhusiano wao wa kibiashara.
Martin Kadinda amesema kuwa kwasasa yeye sio Meneja wa msanii wa Filamu, Wema Sepetu anafanya kazi na msanii huyo kama kaka yake Lakini sio Kama zamani.
Kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online, Martin Kadinda amesema kuwa popote Wema Sepetu atakapo muhitaji kwa msaada au ushauri nini afanye huwa ana mshauri.
Mimi sasa hivi nafanya kazi na Wema kama kaka ake, i do everything popote anapohitaji msaada kuanzia ushauri what to do huwa namshauri lakini mambo mengine binafsi anafanya yeye mwenyewe, mimi kwasasa hivi ni ndugu yake sio Manager”.
Mwezi uliopita Wema Sepetu alikumbwa na skendo ya kusambaza picha zake za faragha akiwa na mpenzi wake katika mitandao ya kijamii.