Mapya Yaibuka Gari Jipya la Diamond

Inasemekana kuwa siku chache baada ya zari kuweka gar lake jipya katika mitandao ya kijaMii, mzazi mwenzie pia Diamond Platinumz alionekana ku-panic na kuamua kurushia ndinga jipya katika mtandao wa kija ii ili kuonyesha kwamba na yeye analipiza kisasi ka mwanamke wake huyo ambae wameachana.

Lakini siri imekuja kufichuka na kusemekana kuwa kumbe gari hiyo aliyoweka Diamond na kusema jipya wala halikuwa jipya bali gari hiyo ilibadilishwa tu muundo na muonekano na moja ya gereji yenye utaaramu huo jijini Dar.

download latest music    

Baada ya Diamond kuanika ndinga hiyo, kampuni ya gpl waliamua kuwatafuta kampuni waliotengeneza gari hiyo na ndipo walipokiri kuwa ni kweli kuwa walikuwa wakibadilisha muonekano wa gari hiyo huku wakigoma kutaja thamani ya matengenezo hayo.

Kampuni hiyo walisema kuwa kutaja bei ya mambo yote waliyofanya kwenye gari hilo ni kama kutoa siri ya mteja wao wakati sio makubaliano ya kampuni na wateja wao.

kumekuwa na ushindani mkubwa kati ya Diamond na Zari baada ya kuachana hasa katika upande wa utajiri na umiliki wa mali.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.