Mange Kimambi Amshauri Hamisa Asirudi Kwa Diamond Adai Ana Gundu
Mwanaharakati wa Mambo ya siasa Mtandaoni Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa Mobetto asithubutu kurudi tena kwa mzazi mwenzake Diamond Platnumz kwa madai kuwa ana gundu.
Hamisa aliweka wazi kuwa yeye na mzazi mwenzake staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz waliachana Mwanzoni mwa mwezi huu baada ya kuwa pamoja kwa miaka kadhaa.
Lakini baada ya kuachana Hamisa aliingia kwenye mgogoro na Familia nzima ya Diamond ambao waliishia kumtangaza kama mchawi mara baada ya kuwaendea kwa mganga.
Mange Kimambi ameibuka na kumshauri Hamisa asirudiane Tena na Diamond kwa madai kuwa familia nzima ya Diamond ilikuwa inampa gundu tu kwani sasahivi tangu ameachana nao amekuwa akipata madili mengi ya ubalozi.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange ameandika maneno haya:
https://www.instagram.com/p/BoGFxI6larV/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=1o9n4uzj4l67d