Mange Atoboa Siri ya Nyumba ya Diamond Adai Sio Yake

Mwanaharakati wa siasa Mange Kimambi amerudi tena kwenye headlines kwa mara nyingine safari hii amemuumbua msanii wa Bongo fleva Diamond Platnumz kwa kudai nyumba alyotangaza kuimiliki jana siyo yake bali amepangisha tu.

Siku ya jana Diamond alitangaza kupitia ukurasa wake kwamba amenunua nyumba ambayo itatumika kama makao makuu ya WCB na itatumika kama studio mpya za redio na television station mpya anayotaka kufungua hivi karibuni.

download latest music    

Baada ya kitrnd sana na watu kumsifia kununua mjengo huo wa kifahari unaoelekea kuwa wa thamani kubwa sana Mange ameibuka na kuweka wazi kuwa jumba lile sio la Diamond bali linamilikiwa na mrembo anayeitwa Resty ambaye ni mfanyabiashara maarufu Instagram.

                            Diamond Akiwa na Wamiliki wa Jumba hilo

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Mange alifunguka yafuatayo kuhusiana na mjengo huo:

Hii ndio siri ya mjengo mpya wa Wasafi, ile nyumbani ni ya baby daddy wake na Resty anaitwa John huyo John yuko jela kwa sasa. Hiyo nyumba alimjengea huyo mwanaye aliyezaa na Resty, huyo Hailey (Huyo mtoto hapo juu) Nyumba ilijengwa miaka mitano iliyopita na hakuna mtu ambaye amewahi kuishi hapo toka imejengwa ipo maeneo ya Shoppers Plaza ya Mbezi beach karibia na kanisani. Wasafi wameipangisha na pesa za kodi zinatmika kumsomesha huyo mtoto kwa sababu nyumba ipo kwa jina la huyo mtoto… Bababke mtoto yupo jela kwaiyo wakaona nyumba ipangishwe ili kodi imsaidie mtoto. Unaambiwa hiyo nyumba ni matata ngazi zipo gold plated ni balaa tupu! Lakini hata kupangisha ni maendeleo pia sio kila mtu anaweza kupangisha hiyo nyumba, hongera Wasafi”.

Mpaka hivi sasa sio Diamond wala Wasafi hakuna aliyejibu tuhuma hizo za kupangisha nyumba kisha kuupotosha uma kwa kudai kuwa imenunuliwa kwani hata dalali wa hiyo nyumba amefanya mahojiano na vituo mbali mbali na kudai kuwa nyumba imenunuliwa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.