Maneno ya Jux kwa Vannesa Yalivyowafurahisha Mashabiki.
Inaweza ikawa ndio couple bora katika mtandao kwa sasa bongo kutokana na ukaribu wao na mapenzi wanayoonyeshana wote wawili, inaweza kusemekana kuwa nguvu kubwa ya mashabiki inawafanya waendelee kudumu katika mahusiano hayo kwa sababu kipindi wamekosana mashabiki wengi walionyesha kuumia na hata kupaza sauti ili wawili hao warudiane.
Kelele kubwa ya sasa kutoka kwa mashabiki sasa hivini wawili hao kuharalisha mahusiano yao na kufunga ndoa ili kuthibitisha kuwa wapo pamoja muda wote, kila wanapoweka picha katika mitandao mashabiki wamekuwa wakiweka maoni yenye kuonyesha kufurahi kuwaona pamoja wawili hao.
Wikiend hii Jux aliweka picha akiwa na vannesa mdee huku wakiwa katika pozi moja matata la kimahaba ambalo liliwakosha mashabiki wengi wa wasanii hao ambao ni wapenzi , lakini pia kikubwa kilichowavutia ni maneno matamu Jux aliyoyaandika kwa Vannesa Mdee.
Ninachotaka kuona ni tabasamu na furaha yako siku zote #bestfriend alafu don’t change your hairstyle nazipenda saaana.-Aliadika Jux katikaukurasa wake wa instagram.