“Maneno Hayawezi Kueleza ni Jinsi Gani Nakupenda”- Ben Pol
Msanii wa muziki wa Bongo fleva Bernard Paul maarufu kama Ben Pol ameibuka na kumtumia ujumbe mzito wa kimahaba Mpenzi wake Anerlisa.
Siku ya jana Anerlisa alikuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa ambapo ameweka wazi kuwa anafikisha miaka 31 na Ben Pol alimtumia ujumbe mzito ambao ulikuwa na maneno matamu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ben Pol ameweka picha moja na video mbili ambazo zilikuwa zimeambatana na maneno yanayosomeka:
Happy Birthday My Love @anerlisa .. Words Cannot Explain How Much I Love You (Maneno hayawezi kueleza jinsi gani navyokupenda)
, Nakutakia Maisha Marefu Na Furaha. May All Your Dreams Come True..(nakuombea ndoto zako zitimie) #MyQueen
”.