Mama Wema Atoa Lawama Kwa Steve Nyerere Kuhusu Wema Kuhama Chama.
Ni siku chache tangu zimepita tokea mama mzazi wa msanii Wema Sepetu kuonekana nchi Kenya alikoenda kumsalimia Mh. Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana, Mama Wema akiwa kama mkereketwa wa chama hicho ambae alihamia Chadema akitoka CCM mwanzoni mwa mwaka huu akiwa na mwane Wema Sepetu,lakini hali imebadilika juzi ambapo Wema Sepetu alitangaza kurudi CCM akitokea Chadema alikohamia hata mwaka haujapiata na kusema kuwa hakuwa akujisikia amani akiwa Chadema na ameamuakurudi nyumbani.
Mama Mzazi wa Wema Sepetu amefunguka na kuongea na waandishi wa habari baada ya tukio ilo kutokea na kusema kuwa yeye hana mpango wa kuhamia CCM tena na anamlaumu sana Steve Nyerere ambae amekuwa akimshawishi vitu vibaya mwanae.
Napenda nitamke wazi kuwa Wema ni mtu mzima na anayajua mwenyewe maamuzi yake,jana nimehamini kweli Wema anahama Chadema na anahamia CCM na safari ya siasa ina mambo mengi sana,napenda nitamke wazi kuwa sina mkakati wowote wa kuhama Chadema ,nitabaki kwenye mabadiliko ya upinzani kwani mabadiliko ni muhimu sana katika nchi yetu.sio vibaya yeye akienda CCM ,mwingine akaenda ACT,na mimi nikabaki chadema na mwingine akawa hana chama kabisa.
Ukimpta mtu kama Steve ni bomu, mimi nitaendelea kuwa mama wakati Wema amekamtwa Central Steve hakuja hata kumjulia hali, lakini leo anashangilia Wema kurudi CCM,Chadema walikuja nyumbani kwangu wakaja kutujulia hali kipindi cha matatizo,walimsaidia Wema mambo mengi ambayo ni sawa wamenisaidia mimi pia , chadema ni familia moja na mimi siwezi kuihama.Alisema Mama Wema Sepetu alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusu msimamo wake wa yeye kurudi CCM