Mama Salma Kikwete Alia na Simu Kwenya Harusi ya Kiba-Square
Mke wa rais mstaafu , mama salma kikweta siku ya jana alibahatika kuongea jambo katika harusi ya ali kiba na mdogo wake abdul kiba iliyofanyika jijini Dar katika ukumbi wa Serena, harusi ambazo zilifungwa siku kadhaa zilizopita na sherehe kufanyika April 29.
Akitoa wosia wake, Mama Kikwete aliwasihi na kuwahasa sana maharusi hao kuhusu matumizi ya simu na mahusiano yao kwa sababu simu zimekuwa zikiharibu ndoa nyingi sana.
Simu ni mtihani na ni hatari sana, mkiendekeza simu mnachukua mnaaangalia , mtaachana siku si nyingi sana,aminianane, mkiaminiana maisha yanakuwa mazuri sana.lakini kila muda ukirudi basi unarudi unaanza kupekua simu ya mwenzako nani katuma meseji, hapana.wakati mwingine simu inalia unaanza kukosa amani mara unatoa nje au unainga chooni kwa ajili ya kuongea.