“Mama Ni Shabiki Wangu Mkubwa”- Young Killer
Msanii maarufu wa hip hop nchini Kassim Yusuph ‘Young Killer’ amefunguka na kuweka wazi kuwa mama yake mzazi ni shabiki wake mkubwa wa kazi zake za kisanii.
Young Killer ‘Msodoki’ amesema mama Yake shabiki wa kazi zake kiasi ya kwamba anaweza kuflow ‘Kurap’ nyimbo zake zote.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Young Killer amesema kuwa kitendo hicho kinamfanya azidi kumpenda mama yake huyo ambaye pia amekuwa akimpa sapoti kwenye mishe zake za kimuziki.
Naweza kusema mama yangu ni shabiki wangu namba moja, ananisapoti kwa kila hali lakini pia hata nyimbo zangu zote anazi-floo fresh kabisa, ni mtu muhimu sana kwangu”.
Lakini pia Young Killer ameweka wazi kuwa ni muhimu kwake kupata sapoti ya mama yake kwani ni kama baraka inayomsaidia kufanikiwa zaidi katika kazi zake.