Mama Mzazi Wa Lulu Diva Atoa Siri Nzito Kuhusu Binti Yake
Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Lulu Abbas maarufu kama Lulu Diva amefunguka na kutoa Siri kuhusu binti yake na kwa kudai kuwa alikuwa anapenda kula kuliko kusoma.
Mama wa Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ kufunguka siri ambayo hajawahi kuisema popote, kwamba katika ukuaji wa mwanaye alikuwa anapenda sana kula kuliko shule.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Ijumaa Wikienda, Mama wa mrembo huyo alisema kipindi Lulu anasoma shule ya msingi alikuwa anapenda kumfungia chakula ili aende nacho shule lakini matokeo yake alikuwa akifika shule anaanza kula kile chakula, kikiisha kabla ya masomo anarudi nyumbani bila kuingia darasani.
Huyu Lulu alinisumbua sana, huwezi kuamini alikuwa anapenda kula kuliko masomo, nilikuwa nikimuandalia ‘paseli’ ya chakula kwa ajili ya kula ikifika mapumziko shuleni lakini cha kushangaza yeye alikuwa akila kabla na kikiisha anarudi nyumbani“.
Lulu Diva Hivi sasa anafanya vizuri kwenye muziki hasa kwenye tasnia ya Bongo fleva ambapo ni mmoja kati ya wasanii wakubwa wa kike Tanzania huku akiwa ametoa kibao kilichofanya vyema mwaka jana kinachoitwa ‘Ona’.