Mama kanumba Aomba Msaada Katika Siku ya Kumbukumbu ya Mwanae
Mama mzazi wa msanii marehemu Steven Kanumba amemuomba msaada mwanadada mwenye asili ya kiuzungu aitwa mouna ili kumsaidia katika kufanya kumbukumbu ya siku ya kifo cha mwane steven ambacho kilitokea mwezi april tarehe 7.
Mama kanumba anasema kuwa amezunguka sehemu mbalimbali kwa ajili ya kupata msada kwa ajili ya kufanya kumbukumbu ya mtoto wake lakini amekwama hivyo amemuona mzungu huyo kumsaidia ili kufanya kumbukumbu hiyo.
Mzungu huyo ambae aliripotiwa kufika tanzania siku kadhaa zlizopita alifika katika kaburi la marehemu Kanumba na kumpa heshima zake na pia aliweza kukutana na familia ya marehemu.
niliona ni bora nimuombe yeye anisaidie maana alikuja tanzania kuniona na pia kuona kaburi la marehemu,hivyo anaonekana kabisa kwa jinsi gani alikuwa na mapenzi ya kweli na mimi. hivyo na mimi nimemuomba kama mwanangu. -Aliongea mama kanumba alipokuwa akifanya mahojiano na Mama Kanumba.