Mama Diamond Amwaga Povu Kulinganishwa na Mobetto
Mama mzazi wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz, Bi. Sandrah maarufu kama Mama Diamond amemwaga Povu zito baada ya mashabiki wa mtandaoni kumlinganisha na aliyekuwa mkwe Wake Hamisa Mobetto.
Sakata hilo lilitokea siku chache zilizopita baada ya Mama Dangote kuweka picha mtandaoni zilizomuonyesha akiwa amebebwa na Mume Wake Shamte ndipo mashabiki walimtuhumu kwa kumuiga Mobetto.
Siku za nyuma kidogo Mobetto aliweka picha zake na Mpenzi Wake Josh Adeyeye zilizomuonyesha wakiwa wamebebana kimahaba ndipo walipounganisha na zile za Mama Dangote na kumtuhumu kwa kuiga.
Katika mahojiano yake aliyofanya Global Publishers, Mama Diamond alimwaga Povu zito Baada ya kuulizwa kuhusu tuhuma hizo:
Unajua siwezi kujibu swali hilo la ajabu, kwani wewe ukibebwa unajisikiaje? Na hayo mambo ya Mobeto jijibu mwenyewe na uandike unachojisikia“.