Mama Ashura Awapa Makavu Mashabiki Wa Alikiba
Msanii chipukizi wa vichekesho kutoka katika kundi la Timamu nchini Tanzania anaejulikana kama Mama Ashura amefunguka na kuwatolea mapovu mashabiki wa Team Alikiba ambao wanajifanya wanampenda sana msanii huyo kumbe ni uongo.Msanii huyo ambae kipindi cha nyuma kabisa alishawahi kuandika katika mtandao wake wa Instagrma maoni yake kuhusu Alikiba na kumtolea mapovu msanii huyo kuhusu tabia yake ya kukaa muda mrefu bila kutoa wimbo ni tabia inayowachosha mashabiki wake, lakini badala yake baadhi ya mashabiki hao wa alikiba walikuja juu na kuanza kumtukana msanii huyo wa vichekesho na kujikuta akiingia katika bifu zito la kimtandao wa watu wanaojiita kama Team Kiba.
Alipokuwa katika mahojino na Times Fm, Mama Ashura amefunguka na kusema kuwa mashabiki wengi wa msanii Alikiba hawako real kama yeye anavyodhani bali wanamshabikia kwa sababau ni maadui wa Diamond, hivyo mashabiki hao wanaona njia ya kumuumiza Diamond ni kumsahabikia Alikiba na kuongeza idadi.Hata hivyo Mama Ashura anasema kuwa hata hao mashabiki wenyewe Alikiba hawajui ” hao mashabiki wenyewe Alikiba hawajui, alafu hawapi hata sapoti, mashabiki wa Alikiba sio wale wa real kabisa, ni maadui wa Diamond” anafunguka Mama Ashura
“Wengi wanakuja kwa alikiba na ku-take advantage, huyo ambae yupo tofauti na huyo lakini wangekuwa real wasingekuwa wanatumia matusi katika mitandao kama njia ya kumsapoti msanii wao” aliongezea msanii huyo wa vichekesho
Hata hivyo Mama Ashura alisena kuwa yeye sio team ya msanii yoyote kati ya Diamond na Alikiba ila tu aliongea kama maoni yake na ushauri kwa Alikiba na mashabiki wake,kwa kuongezea Mama Ashura anasema kuwa inabidi msanii awe na shukrani pale ambapo mtu anafanya kitu kwa ajili ya kazi yake na kutoa ushirikiano kwa watu wanaotoa sapoti kwake katika mitandao ya kijamii “Eric Omond alitoa Cover ya Zilipendwa ya Wasafi na akatoa Seduce Me ya Alikiba lakini Diamond alicomment ‘Asante’ kwa Omondi lakini Alikiba hakufanya hivyo” aliongezea msanii huyo