Makabila Yanayojulikana Sana Afrika.
ZULU.
Hili ni kabila kubwa sana afrika ya kusini lenye karibia watu milion 11 , hili ni kabila kubwa na linalojulikana sana afrika kote.hili ni moja ya kabila ambalo hata watalii huweza kusafiri na kuja kuangalia kama kivutio cha utalii.
YORUBA.
Umati wake unakaribia milion 35 ya watu wake, watu hawa wanapatikana sana katika nchi ya Nigeria lakini pia kusini mwa Benin.
OROMO.
Hawa ni kabila kubwa pia na wanapatikana upande wa kusini wa Ethopia, kaskazini mwa kenya na pia baadhi ya sehemu ya nchi ya Somalia..hili ni kabila kundi kubwa kwa nchi ya Ethiopia ,ambapo karibia ya 35% ya watu wa Ethiopia ni kabila hili.
MASAI
Kabila hili linasifika sana kwa kutunza mila zao na desturi, hata kama watu wake wengine wamesoma na kupata elimu lakini kuna baadhi ya mila zao ni vigumu sana kuziacha .mavazi yao huwa nimashuka na urembo wa shanga, lakini bado wengi wao wanaishi katika nyumba za pamoja kama ukoo zinajulikana kama maboma.
HAUSA
Hili pi ani kabila kubwa na limesambaa sana katika nchi nyingi afrika, unaweza kuktana na kabila hili katika nchi za Sudan, Niger, Nigera,Chad, Togo, Coted’ivore and Ghana, wanaume kwa wanawake wana aina yao ya uvaaji kulingana na jamii pia rangi za nguo zao uendana na mila na desturi zao.
HIMBA
hili ni kabila lingine kubwa linapatikana Afrika , wanapatikana sana kaskazini mwa namibia, na wamekuwa wakijihusisha sana na kilimo lakini pia ufugaji. Wanajulikana sana kwa jina la waafrika wekundu kutokana na muonekano wao wanaojitengenezea baada ya kupata udongo na mafuta yenye rangi hiyo.