Maisha ya Sasa Hayahitaji Mwanamke Mzuri Bali Mwenye Akili :-Irene Paul
Mwanadada kutoka katika kiwanda cha bongo movies Irene Paul amefunguka na kusema kuwa kwa maisha ya sasa jinsi yalivyo hapahiytajiki kuangalia uzuri wa mwanamke ni upi zaidi ya kujua kama mwanamke ulienae ana akili na anaweza kukusaidia katika maisha.
kwa kujitolea mfano yeye mwenyewe anasema kuwa , amekuwa mtu wa kuchukia sana kutegemea kila kitu kutoka kwa mwanaume hivyo anapambana kila kukicha ili waweze kuasaidiana kimaisha kwa vitu vidogo vidogo.
akiongea na dizzim online, Irene anasema “tunaenda kisasa zaidi, maisha ya sasa hayataki mwanamke mzuri hata kidogo, maisha ya sasa yanataka mwanamke mwenye akili, mwanamke anaeweza kutafuta,mimi nikiwa kama mke na kama mama siwezi kumtegemea mme wangu kunileta kila kitu, iswezi kusema kuwa yeye ndio afanye kila kitu, vitu vingine tunasaidiana.”