Maisha Ya Mzee Majuto Matatani,Asakwa Na Wasiojulikana

Inadaiwa kuwa ni siku kama kumi zimepita tangu itolewe taarifa  kuwa msanii wa maigizo na vichekesho nchini Mzee Majuto alipotapeliewa fedha zake na kampuni mojawapo hapa nchini  inayohusika na filamu.Akimuelezea Waziri wa habari Mzee Majuto alidai kuwa kwa sasa hali ya maisha yake iko mashakani baada  ya watu hao wasiojulikana kutaka kumuuua kwa sbabau tu amekuwa akidai haki yake.

Akielezea sakata hilo moja ya watu wa karibu kutoka Tanga ambae akutaka jina lake litajwe alidai kuwa ;

download latest music    

Mzee Majuto hana amani kwa sasa , amekuwa akilalamika kuwa kuna watu wanataka kumuua kwa kuwa alikuwa anadai ela zake ambazo mpaka sasa hajapatiwa hata shilingi kumu na yupo tu hajui cha kufanya, mbaya zaidi ni kwamba alipoteza simu yake kwaio hana wa kuwasiliana nae kumsaidia kwa hilo.kwaio kuogopa kwake kunamfanya anyamaze tu sasa hivi.

Akiulizwa na waandishi kutoka kampuni ya Global alipofuatwa nyumbani kwake, Mzee Majuto alikiri kuwa kweli kuna watu wamekuwa wakimtishia kumnyonga na kumpiga risasi lakini hana ufahamu na watu hao.

Licha ya kumweleza waziri lakini mpaka sasa sijapata kitu changu chochote kwa siku,na ninaogopa kuendelea kudai kwa sababu ninatishiwa kuuawa,si unajua siku hizi mtu ukidai haki zako unaweza kunyongwa au ukiwa barazani  unashtukia unapigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nilikuwa na namba za waziri na nilimpigia baada ya siku ile kunihaidi atashughulika swala langu,lakini siku ile aliniambia yupo kwenye kikao nimtafute wakati mwingine.Siku chache baadae nikiwa nasafiri kwenye ndege nilipoteza simu kwaio nikawa sina namba tena,imebidi nitulie nimwachie mungu tu  atanilipa hizo fedha ninazodai maana naogopa kunyongwa jamani.

Hata hivyo bado Mzee Majuto anamkumbusha na kumuomba Waziri  mwenye mamlaka hiyo kushughulikia swala lake kwa sababu peke yake anaona ameshindwa kabisa.Mwisho wa mwezi uliopita Waziri wa habari alikutana na wasanii na kuzungumza nao ili kujua changamoto zinazowakabili, na katika mazungumzo yake alihaidi kushughulikiwa watu wote ambao wamekuwa wakiwadhulumu na kuwaonea wasanii katika kuwapatia haki zao.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.