Maimatha Afunguka na Kueleza Jinsi Urembo Uivyotaka Kumuumbua Leba
Mtangazaji mkongwe na Msanii Maimartha Jesse amefunguka na kueleza jinsi licha zake za Bandai zilivyompa tabu alipoingia leba miezi Michache iliyopita kwa ajili ya kujifungua mtoto wake.
Maimatha amefunguka na kuweka wazi kuwa moja ya changamoto aliyokutana nayo alipoingia leba kwenda kuzaa akiwa na kucha zake feki na ndefu za kubandika (tips) na kuwapa somo mastaa wanaopenda kubandika kucha kipindi cha ujauzito.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Risasi Jumamosi, Maimartha alisema mara baada ya kuingia leba ilibaki kidogo afukuzwe na daktari kwani kucha alizokuwa amebandika zilikuwa zinageuka kuwa kero na kujikuta akizitoa kwa meno licha ya kwamba alikuwa akipata maumivu makali.
Yaani sitasahau maana kidogo tu nifukuzwe leba kisa kucha za kubandika, niwape tu tahadhari wenzwangu kuwa makini na kucha hizo maana siyo nzuri kabisa“.