Maimartha- Siwezi Kuyumbishwa na Maneno Ya Watu
Mtangazaji mkongwe Maimartha wa Jesse ameibuka na kudai Kuwa hawezi kuyumbishwa na maneno ya watu ambao wamekuwa wakimsema na kumtukana kutokana na yeye kuwa mmbea kwenye mitandao ya kijamii kwani ndio kazi inayomuweka mjini.
Kwenye mahojiano aliyofanya na gazeti la Risasi Jumamosi, Mai alisema kuwa kila akitupia habari yoyote kwenye ukurasa wake wa Instagram watu wanamtukana na kumuita m’mbea, wengine wanadiriki kumwambia auze biashara zake lakini wanasahau kuwa kazi hiyo ameisomea na anahabarisha kama wengine wanavyohabarisha.
Unajua utangazaji ni sawa na umbea, mimi nahabarisha watu kwa staili yangu na sitokoma kazi hii labda watu wafiche mambo yao lakini hivi hivi sikomi, ni kazi kama kazi nyingine”.
Mai amemwaga povu hilo baada ya siku za hivi karibuni kuingia matatizoni na baadhi ya mashabiki wa wasanii mbali mbali hasa Hamisa Mobetto baada ya kuivalia njuga ishu ya Hamisa kuwa na mpenzi mpya.