Maimartha Ang’ang’ana Na Hamisa Mobeto.
Mwanadada ambae ni moja ya watangazaji maarufu nchini Maimartha wa Jesse ameibukana kusema hata kama Hamisa Mobeto amekaa kusikiliza ushauri wake hatokaa aache kumfunda kwa sababu yeye anamuonea huruma kwa sababu badala ya kutenga muda kwa ajili ya familia yake na kufanya mambo yake ya maendeleo amekuwa akifanya vitu ambavyo vinamfanya kushindana na Zari katika mitandao ilhali mwanamke anaeshindana nae anamzidi kwa kila kitu.
Mara ya kwanza Maimartha aliandika katika ukurasa wake wa instagram na kumshauri Hamisa kuacha kurumbana na Zari kwa sababu kwanza anakuwa anamuumiza mama yake kwa kuwa anatukana matusi na Team Zari lakini pia angeachana na kukubali matokea kuwa Diamond hawezi kumuoa kwaio ampende na kupatana na Zari ili aweze kulea mtoto wake vizuri.
Lakini kitu cha ajabu ni kwamba hamisa hakutaka kuupokea ujumbe huo kama ambavyo maimartha alihisi angeweza kuupokea zaidi ya kumwambia kuwa ushauru huo angeufanyia kazi kwa familia yake.
Mairmatha alisema kuwa pamoja na majibu mabaya ya Hamisa lakini bado yeye hatoaacha kumshauri kwa sababu anaona kabisa kuwa anapotea. Lakini pia anaamini kuwa hata kama anamjibu vibaya lakini meseji anazompa anazisoma na anajifunza kitu hata kama hataki kuonyesha kuwa anajali.
Kiukweli niliamua kumshauri na nitaendelea kumshauri ingawa yeyey alinijibu vibaya, ila ninachoamini ni kwamba ujumbe unamfikia na anatakiwa kujirekebisha tu na ni kweli lile tamasha halikuwa ya hadhi yake.