Mafanikio Ya Lulu Michael Yazidi Kuonekana
Msanii wa filamu nchini Elizabeth Lulu Michael, anazidi kuonyesha mafanikio anayoyapata katika kazi zake baada ya kupata tena donge nono kutoka katika televisheni ya Sinema Zetu inayopatikana Azam Tv inayohusika na filamu za Afrika Mashariki.Msanii huyo wa kike ambae pia ni moja wa warembo wanaosifika kwa kupendeza Bongo na inawezekana ndio msanii wa kike anaewazidi wasanii wengine, amesaini dili nono la kuwa balozi wa (SZIFF) Sinema zetu international festival kwa mwaka 2017/2018.
Msanii huyo wa kike ambae mwaka jana (2016) alipata tuzo ya AMVCA katika kategoria ya filamu bora ya mwaka kupitia filamu yake iliyojulikana kama ‘Mapenzi ya Mungu, alidhirisha kuwepo kwa mkataba wake na Sinema Zetu kwa kuandika maneneo ya kuwashukuru watu hao na kuwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kukuza filamu za Afrika.
Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram kuelezea kwa undani juu ya tamasha ilo ambalo limeanzishwa na Azam Tv kupitia channeli ya Sinema Zetu lenye lengo la kutoa Tuzo kwa Filamu za Afrika Mashariki Lulu Michael aliandika “Oct 2/2017….Azam tv kupitia channel ya Sinema Zetu imezindua rasmi tamasha la tuzo za filamu kwa upande wa Afrika Mashariki SINEMA ZETU INTERNATIONAL FESTIVAL (SZIFF).Hizi ndizo tuzo zitakazo husisha waandaaji na wadau wa Filamu Tanzania .Ni Tuzo za Filamu kupitia Televisheni zenye nia ya kuleta Mapinduzi katika soko la Filamu nchini Tanzania ” alifunguka kwa undani.
Pia alionyesha shukrani zake za dhati kwa waandaji wa filamu izo kwa kumchagua yeye kuwa kama balozi kwa tanzania kuwakilisha wadau wengune wa sanaa “Nitoe shukrani zangu za dhati kabisa kwa uongozi mzima wa azam tv kwa heshima niliyopewa ya kuwa balozi wa tuzo hizi.hii ikimaanisha kuwakilisha tasnia nzima ya filamu katika tuzo hizi.” aliongezea Lulu.
Hata hivyo Lulu alichukua jukumu la kuwa kama balozi kuhamasisha wadau wote na waandaaji wa Filamu nchini kujitolea kushiriki katika tuzo izo “mwisho nitoe kwa waandaaji pamoja na wadau wa filamu kufatilia na kushiriki katiak tuzo hizo. CC@ sinema zetu #hakikanizakwetu” alimalizia Lulu.Pongezi nyingi zimfike Lulu Michael!!!!