Mafanikio Ya ‘Iokote’ Yampelekea Maua Sama Kuporomosha Mjengo
Msanii wa muziki wa Bongo fleva ambaye mwaka jana alifanya vyema na wimbo wake wa ‘Iokote’ amefunguka na kusema nguvu ya mashabiki katika kumpa sapoti kumemsaidia kuweza kununua gari na sasa kujenga Nyumba.
Maua Sama ambaye siku si nyingi aliweka wazi gari aina ya Toyota Rav 4 ambalo alikiri kuwa alinunua kutokana na wimbo wake wa Iokote kufanya vyema Lakini sasa amesema ameweza kununua kiwanja kwa ajili ya kujenga Nyumba yake.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Gazeti la Risasi Mchanganyiko, Maua Sama alisema kuwa kwa sasa ameanza ujenzi wa ‘bangaloo hatari’ maeneo ya Mbweni jijini Dar.
Mashabiki wangu ndiyo wamenipa mafanikio na kunifanya niweze kununua kitu ambacho nakitaka, hata hili gari limetoka kwao hakuna mtu mwingine zaidi ya mashabiki wangu na nipo mbioni kumalizia mjengo wangu kwa nguvu zao”.