Mafanikio Hayaambukizwi Kwa Njia Ya Kujaamina- Zari
Mwanamama mfanyabiashara maarufu Zarinah Hassan ‘Zari The Bosslady’ amewatolea povu zito wasichana ambao amedai ni wadangaji na kuwaambia mafanikio hayapatikani kwa njia ya kujaamiana.
Zari alitoa povu hilo siku chache zilizopita alipokuwa anamkumbuka Ex wake Ivan Semwanga aliyefariki dunia mwaka jana kutokana na maradhi ya ugonjwa wa moyo.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Zari aliandika ujumbe huo:
Pale unaposikia pesa za urithi…apo vipi Mafanikio hayaambukizwa kwa njia ya kujaamiana. .Endeleeni kudanga mkafikiri mwanaume tajiri atatokea man kukupa utajiri wa ghafla, na hata kama akiweza wewe utakuwa kama pambo ambalo anaweza akalitupa akinunua jipya lakini mimi sio rahisi kunitupa kwa maana mimi ni msingi na sio paa”.
Zari alitoa povu hilo baada ya kudaiwa pesa alizonazo ni za Marehemu Ivan na sio Mali yake lakini Zari alianika picha zake za zamani na Ivan na kuwajulisha watu wakati anaanza uhusiano na Ivan alikuwa hana hizo Mali hivyo walichuma wote.